Waigizaji maarufu wa kike wa Hollywood watashiriki maandamano mjini Washington January 21, siku moja baada ya Donald Trump kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Marekani, maandamano hayo yataongozwa na Chelsea Handler, kuanzia katika eneo la Park City jimbo la Utah,

Waigizaji hao maarufu nchini Marekani wailalamikia serikali ya Trump kwa kuingilia uhuru wa wanawake na kufanya maamuzi kuhusu uzazi na utoaji mimba, Pia wailalamikia tangu uchaguzi ukamilike watu wengi wanahofia sauti zao kutosikika.

America Ferrera ambaye ni mwigizaji wa kipindi cha Ugly Betty, aliyemuunga mkono Hilary Clinton wa chama cha Democratic amesema anashiriki maandamano hayo na kuhakikisha sauti yake inasikika na “kusimamia kile anachokiamini”.

Waigizaji wengine wa kike watakaoshiriki ni pamoja na Amy Schumer, Scarlett Johansson, Frances McDormand na Zendaya, Uzo Aduba wa The New Black, Lea DeLaria na Diane Guerrero. Wengine watakaoshiriki kupitia njia zingine kuunga mkono mpango huo ni Katy Perry, Julianne Moore, Cher na Debra Messing.

”Kama wasanii, wanawake na zaidi ya yote Wamarekani waliojitolea ni muhimu tushirikiane kulinda hadhi ya jamii yetu.” amesema America Ferrera.

 

Video: Nape amkabidhi bendera ya Taifa Diamond kutumbuiza AFCON 2017, nchini Gabon
Serikali yakamilisha mkakati wa magonjwa yasiyo ambukiza

Comments

comments