Serikali nchini, imetoa takwimu za wajane Duniani ambazo zinaonesha wengi wao hudhulumiwa na kunyimwa haki zao wakiwemo wanaoishi kwenye mazingira duni, huku Tanzania ikiwa na wajane zaidi la laki nane, wanaoomba kufanyiwa kwa mabadiliko ya sheria za mirathi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma hii leo Juni 22, 2022 katika maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wajane Duniani kinachotarajiwa kufanyika hapo kesho Juni 23, 2022.

“Inakadiliwa kuwa duniani kuna wajane Milioni 258, ambapo 115 Milioni kati yao hudhulumiwa na kunyimwa haki zao za msingi huku na mjane mmoja kati ya 10 akiwa anaishi kwenye mazingira duni kupitiliza,” ameeleza.

Waziri Gwajima amesema, Serikali imeanza kutokomeza mila na desturi kandamizi kwa wajane, ili kuokoa maisha na maslahi ya watoto wanaoachwa bila mzazi mmoja.

“Wajane wana changamoto zao na bado jamii inawanyanyasa kwakua wanaonekana ni kundi lisilo na muhimu na wenza wao tayari hawapo duniani hivyo familia nyingi zinasambaratika na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani,” amesema Waziri Gwajima.

Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA), Rose Sarwatt ameiomba Serikali kufanyia marekebisho ya sheria ya mirathi, kwakua wajane wengi bado wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kunyanyaswa, kuteswa na kulazimishwa kuolewa na ndugu wa marehemu.

“Serikali iangalie uwezekano wa kufanyia maboresho sheria ya mirathi, maana wajane wengi bado wanakumbwa na changamoto za kunyanyaswa, kuteswa, kulazimishwa kuolewa na ndugu wa marehemu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha, amebainisha kuwa changamoto zingine ni pamoja na wajane hao kudhurumiwa haki zao na wengine kunyanyapaliwa na ndugu au jamaa na wananchi, mara baada ya kufiwa na wame zao.

Katika hatua nyingine, Dkt. Gwajima amesema tayari wameanza kutokomeza mila na desturi kandamizi kwa wajane, ili kuokoa maisha na maslahi ya watoto wanaoachwa bila ya mzazi mmoja, hali inayochangia umaskini kwenye jamii.

Ombi la akina Mdee ladunda
FIFA yaiadhibu Biashara United Mara