Wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya, wamesema kuwa, wana mashaka iwapo Myanmar ina nia ya dhati ya kuwakaribisha nyumbani kwao, baada ya msemaji wa uongozi wa kijeshi nchini humo kusema kwamba wataanza kukaribisha kundi hilo la walio wachache kuanzia mwezi ujao wa Aprili.

Ujumbe wa maafisa 17, kutoka kundi la kijeshi linalotawala nchini Myanmar umetembelea Bangladesh wiki hii ili kufanya mahojiano na baadhi ya wakimbizi, ambao huenda wakarejea, ikiwa ni miaka 5 baada ya kufanyika msako mkali wa kijeshi uliopelekea idadi kubwa ya kabila la Rohingya kuyakkimbia makkazi yao.

Ziara hiyo iliyoongozwa na China na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa inaashiria kuanza kwa makubaliano kati ya Maynmar na Bangladesh, ya kuwerejesha wakimbizi baada ya muda mrefu wa wasiwasi kwamba wangeteseka iwapo wangerejea makwao.

Hata hivyo, baadhi ya wakimbizi hao wa Kirohingya wameziambia duru za habari kwamba hawakupata majibu ya kuridhisha kuhusu haki zao za uraia wa Myanmar.

Wakimbizi hao, ambao ni Waislamu wa jamii ya Rohingya walioko katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh, wanakabiliwa na hali mbaya na hata hatari ya kifo kutokana na kupunguzwa misaada waliokuwa wakipatiwa.

Maelfu ya Waislamu hao nchini Myanmar, wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa tangu kuanza wimbi jipya la mashambulizi ya jeshi na Mabudha wenye misimamo mikali katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi nchi hiyo tangu tarehe 25 Agosti mwaka 2017 hadi sasa.

Mauaji hayo ya umati dhidi ya Waislamu nchini Myanmar yamepelekea zaidi ya nusu milioni kati yao kukimbia nchi yao na kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Southgate aweka wazi hatma yake England
Dunia ishikamane mapambano dhidi ya Kifua Kikuu