Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametangaza kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), akiwemo Mkurugenzi wa wa Kanda, Huduma kwa Wateja wa Bodi hiyo, Cosmas Mwaifwani kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.5.

cosmas

Cosmas Mwaifwani

Waziri Mwalimu ametangaza hatua hiyo leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akikabidhi vitanda kutoka MSD kwa ajili ya kuwekwa kwenye jengo la hospitali hilo kutekeleza maagizo ya Rais John Magufuli ya kulibadilishia matumizi jengo hilo kutoka kuwa ofisi ya maafisa wa Wizara ya Afya na kuwa Wodi ya Wazazi.

Watumishi wengine waliosimamishwa kazi kufuatia sakata hilo ni pamoja na Mkurugenzi wa fedha, Joseph Tesha, Mkurugenzi wa ugavi Misanga Muja na Mkurugenzi wa manunuzi, Henry Mchunga.

Alisema watumishi hao wa umma wanasimamishwa mara moja ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa kiasi hicho kikubwa cha fedha zinazowakabili.

 

Rais Magufuli awateua Mabalozi wapya, awapandisha vyeo Polisi na kuwapangia kazi mpya
Matola Atuma Salamu Ligi Kuu Msimu Wa 2016-17