Jumla ya watu 57 waliokuwa wanashikiliwa mateka na kundi la waasi la Allied Democratic Forces-ADF, mashariki mwa Kongo wamekutanishwa na familia zao hapo jana Jumamosi Desemba 3, 2022.

Miongoni mwa watu hao ni pamoja na wanawake waliokuwa wakitumiwa kama watumwa wa vitendo vya ngono, ambao waliachiliwa huru mwishoni mwa juma baada ya operesheni kubwa ya kijeshi baina ya wanajeshi wa Kongo na Uganda.

Moja kati ya raia ambao wameamua kuyahama makazi yao kutokana na mapigano inayoemdelea mashariki mwa DRC. Picha ya VOA.

Oparesheni hiyo iliwapa wanawake hao nafasi ya kutoroka mikononi mwa ADF, ambapo sherehe ya kuwaunganisha tena mateka hao wa zamani na familia zao ilifanyika katika mji wa Beni, uliopo eneo la Kivu ya Kaskazini.

Kumekuwa na mapigamo ya mara kwa mara katika ukanda wa mashariki mwa DRC, ambao unatajwa kushikiliwa na waasi wa kundi la M23 linalodaiwa kupewa nguvu na Rwanda huku nchi hiyo ikikanusha vikali kuhusika na madai hayo.

Wakaguzi 'wazembe' Serikalini wakalia kuti kavu
Maombolezo vifo vya watu zaidi ya 100