Wanajeshi waliokuwa wamezunguka makazi ya ya kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine, wameondoka baada ya jana Jumatatu Mahakama kuliamuru jeshi na polisi kuondoka kwenye makazi yake.

Bobi Wine hajaondoka kwenye makazi yake yaliyo kando ya mji wa Kampala, tangu alipopiga kura kwenye uchaguzi siku 11 zilizopita.

Waandishi wa habari wa gazeti la Daily Monitor wamesema upelekaji wa jeshi na polisi ulikuwa umeimarishwa kwenye barabara inayoongoza kuelekea kwenye makazi ya Bobi Wine na vituo vya ukaguzi vimeongezeka.

Magari mawili yaliyokuwa yamewabeba waandishi wa habari kuelekea nyumbani kwa Bobi Wine yalizuiwa na waandishi hao kuamriwa kurejea walikotoka.

Bobi Wine sasa ameondoka nyumbani kwake ili kuzungumza na vyombo vya habari.

Waziri awaonya wanaotoa taarifa za wateja makampuni ya simu
Kocha Kaze achukua maamuzi magumu Young Africans