Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeelezea kupokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, baada ya kuripotiwa kuwa wasanii hao watatu wamepata ajali hii leo wakitokea mkoani Iringa.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ameandika:

“Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka” ameandika Polepole.

Balozi wa Iran nchini aagwa
Tanzania Prisons wafichua udhaifu Young Africans