Takribani watanzania 119 waliokuwa wamekwama katika nchi za Falme za Kiarabu baada ya mlipuko wa Corona wamesili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nane mchana kwa ndege ya shirika la ndege la FLY Dubai.

FLY Dubai imewarejesha watanzania hao waliokuwa wamekwama Abu Dhabi tangu 25 machi 2020 mara baada ya serikali ya falme za kiarabu ilipotoa zuio la kuingia na kutoka.

Wakizungumza wakati na  baada ya kumaliza taratibu zote za uhamiaji baadhi ya Watanzania hao ambao wengine walikuwa na watoto wadogo wamesema maisha ya kufungiwa ndani kwa takribani miezi mitatu si rahisi hata kidogo jambo lililosababisha ugumu wa maisha baada ya wengine akiba zao kumalizika.

Ikumbukwe kuwa tarehe 15 may 2020, watanzania takribani 246 walirejeshwa na serikali wakitokea India.

Mganga mkuu wa mkoa ataka Dar ijikinge na Corona

Oxfam kufunga ofisi zake nchi 18 Tanzania yatajwa

Kante ahofia mazoezi Chelsea
Kovu lisilofutika: Miaka 24 kuzama kwa MV Bukoba

Comments

comments