Mamilioni ya watu ambao ni wakazi wa Somalia nchi iliyo katika pembe ya bara la Afrika wanahitaji chakula kutokana na vipindi virefu vya kiangazi kushuhudiwa nchini humo.

Taarifa zinasema mwezi Machi mwaka huu maeneo yote nchini humo yamekubwa na ukame pamoja na vipindi vya joto lisilo la kawaida huku maeneo mengine ya Somali land na Puntland yakiathiriwa vibaya zaidi.

Mvua za msimu maarufu kama Deyr ambazo hunyesha Oktoba hadi Disemba, hazikunyesha kama ilivyotarajiwa mwaka uliopita wa 2018 na hivyo maeneo mengi Somalia sasa yanashuhudia kiangazi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) watu milioni 4.9 kote Somalia wanahitaji misaada ya chakula huku watoto zaidi ya milioni 1.2 wakiwa wahanga wa kukumbwa na tatizo la lishe duni.

Huku hayo yakijiri Idara ya Utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya imeeleza kuwa kimbunga cha Idai katika Bahari ya Hindi ndicho kimechangia pakubwa ukosefu wa mvua katika maeneo mengi nchini humo

Naibu mkurugenzi wa idara hiyo, Ayub Shaka, alisema hali ya kiangazi katika maeneo mengi ya Kenya inatarajiwa kuendelea ijapo kuwa mvua kiasi zimeshuhudiwa katika baadhi ya maeneo. Hali sawa na hiyo inaripotiwa katika nchi za ukanda wa Pembe

Aliyemuua mkewe kwa kumnyima unyumba afia gerezani
Video: Ndugai na CAG ni zaidi ya vita, Spika amtaka CAG ajiuzulu

Comments

comments