Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amekutana na Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC), Collen Kelapile katika kikao kilicholenga kupata maelezo kabla ya kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2022, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ADPA.

Aidha, kikao hicho kinalenga kujadili namna bora za kutumia rasilimali katika nchi husika kuibua maendeleo jumuishi kwenye jamii ambazo maliasili hizo zinapatikana ili zisaidie kuleta amani na hatimaye kufikiwa maendeleo endelevu.

Kikao hicho kitafanyika chini ya mada isemayo ‘Maliasili Jamii yenye Amani na Maendeleo Endelevu: Mafunzo kutoka kwenye Mchakato wa Kimberley’

Wengine wanaoshiriki kikao hicho katika picha ni pamoja na Waziri wa Madini wa Zimbabwe Wiston Chitando ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ADPA, Mratibu wa Kimberly Afrika Jacob Thamage na Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Balozi Prof.
Kennedy Gastorn.

Putin: Operashion ya kijeshi ilikuwa lazima ifanyike Ukraine
Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka mwanafunzi mara bili