Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba ameongoza kikao kazi kilichohusisha Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makatibu Wakuu na Maafisa waandamizi kwa upande wa Tanzania kujadili agenda za kikao kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.

Waziri Mwigulu amepokea taarifa ya agenda za mkutano zitakazojadiliwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi ambaye ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya maafisa waandamizi.

Mawaziri wamepokea na kupitia taarifa za utekelezaji wa vyombo na Taasisi za EAC, zikiwemo Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kamisheni ya Kiswahili ambayo Makao Makuu yake yapo Zanzibar na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maendeleo ya mchakato wa kubadilisha sheria na taratibu za EAC ili kuwezesha kuanza rasmi matumizi ya lugha ya Kiswahili pamoja na Kifaransa kama ilivyoelekezwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Februari 2021 na Mchakato wa uhakiki wa maombi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa mwanachama mpya wa EAC.

Mawaziri wengine waliohudhuria kikao kazi hiki ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Rihanna awa Shujaa wa Barbados
Vanessa Mdee awafumbua Macho wasanii