Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kuwa, wachezaji kutoka nchi za Afrika walikua na umuhimu mkubwa katika kipindi cha miaka 20 ya kazi yake ndani ya klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London.

Wenger alitoboa siri hiyo alipofanyiwa mahojiano maalum na BBC mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari uliokua unazungumzia mchezo wa ligi ya Uingereza dhidi ya Burnley.

Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger alisema wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu kuyapata kwenye mchezo.

Aliwataja wachezaji waliosaidia mafanikio yake ndani ya Arsenal kwa kipindi cha miaka 20 ya kazi yake akiwemo Nwanko Kanu wa Nigeria na Kolo Toure wa Ivory Coast huku akimuongeza gwiji wa Liberia George Weah, ambaye alimfundisha alipokua akikinoa kikosi cha AS Monaco ya nchini Ufaransa.

Wakati huo huo ametunukiwa tuzo ya heshima na uongozi wa klabu ya Arsenal kufuatia kazi aliyoifanya klabuni hapo kwa miongo mwili.

Video: Chadema yafuta Ukuta Oktoba Mosi
Ligi Kuu Ya ZFA Msimu Wa 2016/17 Ipo Mbioni Kuanza