Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imetangaza kuwanasa Watuhumiwa watatu ambao ni Washirika wa Mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy Kambi Zubeir Seif wakiwa na Kilo 15.19 za Dawa za Kulevya Aina ya Heroin.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya amewataja Watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Suleyman Thabit, Sharifa Suleyman Bakari pamoja na Farid Hamis Said wote wakiwa ni Wakazi wa Dar Es Salaam.

“Ukamataji wa Kilo 15.19 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin zilizowahusisha Watuhumiwa watatu ambao ni washirika wa Kambi Zuberi Seif ni muendelezo wa Oparesheni Zilizopita” amesema Kamishna Jenerali Kusaya.

Akizungumza leo Disemba 07, 2022 Jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali Kusaya amesema katika Kipindi cha Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya imefanikiwa kukamata Jumla ya Kilo 16.643 za Dawa za Kulevya zikijumuisha Kilo 15.19 za heroin, gramu 655.73 za Cocaine pamoja na Gramu 968.67 za Methamphetamine zilizohusisha Watuhumiwa Saba.

Chanzo : Wasafi FM

Kesi ya Bin Salman mauaji ya Khashoggi yafutwa
Geita Gold FC yampa uhuru George Mpole