Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto imesema inakusudia kuwasilisha muswada wa sheria mpya bungeni mwakani,itakayowalazimisha wahitimu wa udaktari kupangiwa kwenye kituo chochote cha afya na serikali, ambapo watafanya kazi zaidi ya miaka miwili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Khamis Kigwangala, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari,amesema kuwa huenda muswada huo ukawasilishwa katika Bunge la Februari mwakani.

Kigwangala amesema endapo sheria hiyo itapitishwa na bunge hilo, inakusudia kubadili muundo mzima wa watumishi wa sekta ya afya.

“Sheria hii,itaweka kipindi cha lazima cha National Service(utmishi wa umma) na kila daktari ya anayehitimu kwa sababu amesomeshwa na kodi za watanzania,atalazimika kupangiwa kituo chochote cha serikali ambako atafanya kazi kwa kipindi kisichopungua miaka  miwili kwa lazima”amesema Kigwangala.

Hata hivyo Dkt. Kigwangala amesema kuwa Wizara hiyo ina mpango wa kuhakikisha inarasimisha suala la matibabu bure kuwa kwa makundi maalumu kwa kulitambua kishria, ili liweze kutekelezwa na kuwafikia walengwa.

Polepole atangaza 'vua gamba' ya CCM kivingine
Video: JPM atumbua vigogo 300, Faru John sasa 'kufa' na vigogo....