Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imefafanua kuwa wamefungia kozi ya kujioongezea uwezo (Foundation Course) kwaajili ya kuimarisha mtu kufikia elimu ya chuo kikuu ambayo ilkuwa ikitolewa katika vyuo mbali mbali hapa nchini.

Amesema wamefunga kutolewa mpaka hapo  Serikali itakapopitia upya sheria zilizoanzisha kozi hiyo na kwamba itatafuta utaratibu mwingine na kusisitiza kuwa kujiunga elimu ya juu si kwa wanafunzi wa kidato cha sita pekee bali ni pamoja na wale waliomaliza kidato cha nne waliofuata utaratibu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella manyanya amesema kozi hizo zilianzishwa kwa nia njema,lakini wataangalia ni namna gani watasimamia mfumo huo.

Manyanya amesema elimu ya ziada ilikuwepo na nia yake ilikuwa ni njema isipokuwa haikukaa kwenye mfumo rasmi,hivyo wadau wakubaliane ili iwe inatambulika na kwamba wataendelea kupitia sheria ya vyuo hivyo kuona mapungufu yaliyopo na kuyafanyia marekebisho.

Video: Sakata la kufungwa kiwanda cha Dangote, Waziri Mwijage ataka asiingiliwe
Video: Kikwete asimulia alivyopewa kuku na mzee Xavery Pinda, 'alikuwa mtu mwema sana'