Serikali imewataka maafisa jamii katika halmashauri zote nchini kusimamia utekelezaji wa wizara ya afya katika kupinga vitendo vya kikatili vinavyotokea katika jamii ili kuhakikisha haki za wananchi na makundi tete zinapatikana kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Meandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya vitendo vya kikatili.

“Nitumie nafasi kuwaasa maafisa jamii wote katika halmashauri zote nchini kusimamia utekelezaji wa maagizo niliyotoa na kushughulikia ipasvyo ukatili dhidi ya wanawake,wanaume,watoto na wazee kwa kuhakikisha haki za wananchi wanaoonewa ikiwemo makundi tete,zinapatikana”, amesema Dkt. Gwajima.

“Wanaume msione aibu, muache kukaa kimya dhidi ya vitendo vya ukatili mnavyofanyiwa, toeni taarifa mapema kwa mamlaka husika muweze kupatiwa msaada ili kuzuia madhara zaidi kutokea”, amesisitiza Dkt. Gwajima.

Hata hivyo ametaja sababu zinazosababisha ukatili huu kuwa pamoja na migogoro ya kifamilia ikiwemo kugombea mali, matatizo ya kisaikolojia na jamii kutotekeleza wajibu wake wa kutunza na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amewataka wananchi wote ambao wanaonewa bila msaada wowote kutoa taarifa mapema kwenye mamlaka husika kuanzia ngazi ya mtaa na kupiga simu 116 kwa msaada wa haraka.

Dkt. Gwajima amesema kuwa wizara yake itaendelea kushughulikia ukatili ikiwemo mauaji dhidi ya wazee ambao ni hazina na tunu yataifa inayotakiwa kutunzwa na kulindwa vema kwa manufaa ya maendele ya taifa kamailivyoainishwa katika sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003.

VIDEO: Kisa FIFA, Mwakalebela amrushia mpira kaimu katibu mkuu
'Janja Janja' za mawakala zashtukiwa Simba SC