Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa anakabiliwa na wito wa kujiuzulu baada uchunguzi wa Bunge kubaini kuwa huenda alikiuka sheria za nchi dhidi ya ufisadi kuhusiana na madai ya wizi wa kiasi kikubwa cha fedha zilizopatikana katika shamba lake la Phala Phala game.

Wito huo wa kujiuzulu, umetolewa na wapinzani wake wa ndani katika Chama tawala cha African National Congress (ANC), kufuatia madai ya aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini humo, Arthur Fraser, kwamba Ramaphosa alijaribu kuficha wizi huo wa pesa uliotokea mwaka 2020.

Rais Ramaphosa (picha ya kulia) na sehemu ya mifugo (picha ya kushoto) inayopatikana ndani ya shamba lake la Phala Phala. Picha ya Briefly News.

Kulingana na ripoti hiyo, Ramaphosa alidai pesa zilizoibwa zilikuwa Dola 580 000, na kupinga kiasi cha awali cha Dola milioni 4 milioni ambazo Fraser alidai ndizo ziliibiwa.

Rais Ramaphosa amekuwa akikana kuhusika na lawama hizo na kwamba hana uhusiano wowote na pesa iliyopatikana kwenye shamba lake huku kamati kuu ya kitaifa ya ANC, ambayo ni ya juu zaidi ya kuchukua maamuzi, ikitarajia kukutana kwa dharura.

Rais Samia aipa cheti GGML mapambano ya Ukimwi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 2, 2022