Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya awali Young Africans, huenda wakacheza mchezo wao dhidi ya Rivers United bila Mashabiki.

Young Africans itaanza harakati za kusaka taji la Afrika kwa kucheza nyumbani jijini Dar es salaam Jumapili (Septemb 12), kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Msemaji wa klabu hiyo kongwe katikaa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Haji Manara amesema bado hawajapokea taarifa yoyote kutoka CAF inayotoa agizo la Mashabiki kuushuhudia mchezo huo wakiwa Uwanjani.

Manara amesema wanaendelea kusubiri jibu la CAF, huku akiwataka Mashabiki na Wanachama kuwa wastahamilivu katika jambo hilo ambalo limechukua nafasi kubwa kweye Mitandao ya Kijamii.

“Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka CAF kupitia TFF iliyothibitishwa kuwa idadi ya mashabiki wataohudhiria mchezo wetu dhidi ya Rivers United, kinachoendelea kwenye mitandao kuhusu kuzuiwa kwa mashabiki sio rasmi, Wanayanga wawe wapole wasubiri taarifa rasmi” amisema Manara

FIFA na CAF wameweka marufuku kwa nchi kadhaa duniani kuruhusu Mashabikk kuingia viwanjani kwa kuhofia maambukizi ya virusi vya Uviko 19 (Covid 19).

ATCL waja na kibubu
Tozo mpya yamuamsha Spika