Zaidi ya watu milioni moja katika majimbo nane ya Msumbiji wameathirika ugonjwa wa Kipindupindu, kufuatia madhara ya kimbunga Freddy kilicholeta mafuriko, polio, kuongezeka kwa homa za Uviko-19 na janga la kibinadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva – Uswisi, Mwakilishi wa WHO nchini Msumbiji, Dkt. Severin von Xylander amesema Idadi ya waathirika ni kubwa na kwamba zaidi ya watu milioni moja katika mikoa minane, wanaathiriwa na kipindupindu, mafuriko na Kimbunga Freddy pekee.

Amesema, Kimbunga Fredy kiliharibu zaidi ya nyumba 132 na kusababisha watu 184,000 kukosa makazi huku vituo vingi vya malazi vilivyofungwa vikifunguliwa katika Wilaya nyingi na makazi kwa familia zenye uhitaji.

Wakati wa Kimbunga hicho, pia vituo vya afya 163 viliharibiwa na kuhatarisha upatikanaji wa huduma za kawaida za afya na uharibifu wa dhoruba hiyo kwa huduma za umma na miundombinu umekuwa wa kushangaza, ambapo mafuriko ya mapema Februari, 2023 yalisababisha na mvua kubwa za msimu, na kimbunga Freddy kilipiga mara mbili kwa Februari 24 na Machi 11.

Ntibazonkiza atia neno Ligi ya Mabingwa Afrika
Edna Lema: Nitaweka Rekodi Ligi Kuu wanaume