Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) unatarajia kufanyika leo  Aprili 14 Gombani Wilaya ya  Chakechake kisiwani Pemba, kuanzia saa4 kamili za asubuhi ambapo wadau mbali mbali kujitokeza kuwania nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho.

Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni tatu ambazo ni Rais wa ZFA, Makamu wa Rais ZFA Unguja na Makamu wa Rais ZFA Pemba.

Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Suleiman Haji “Kibabu” amesema matayarisho yote yameshakamilika kuelekea kwenye uchaguzi wa leo wa ZFA.

matayarisho yote yameshakamilika tunachosubiri ufike muda tuanze uchaguzi wetu kwasababu wajumbe kwa asilimia 95 wote wameshafika hapa Pemba na jeshi la polisi tayari lipo kuhakikisha linaweka usalama katika zoezi hili la leo”. Alisema Kibabu.

Katika Uchaguzi huo wa leo jumla ya wagombea 7 ndio waliojitokeza kuwania nafasi 3 zinazowaniwa kwa nafasi ya Urais, Makamu Urais ZFA Pemba na Makamu Urais ZAF Unguja.

Wanaowania Urais wapo wawili ambao ni kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’, Salum Bausi na Ravia Idarous Faina rais anaemaliza muda wake kwenye chama hicho.

Upande wa Umakamu Urais ZFA Unguja wanagombea ni aliekuewa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha CHAUMMA ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Malindi, Mohamed Masoud na Wengine ni Mzee Zam Ali ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa ZFA wakati wa utawala wa Rais Ali Ferej Tamim pamoja na mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ ambae ni Salum Nassor Mkweche.

Na wanaowania nafasi ya Makamu wa Rais ZFA Pemba ni Ali Mohamed Ali ambae anatetea nafasi yake hiyo na Sued Hamad Makame.

Lugumi atoroka nchini usiku wa manane kukwepa rungu la Magufuli
Viporo Vya Young Africans, Azam FC Vyaliwa Kwa Shangwe