Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 29 imemuachia huru Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kwa sharti la kutotoa matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Zitto alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, katika Kesi namba 327 ya mwaka 2018, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018, wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa naneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Kwa mara ya kwanza Zitto Kabwe, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, 2018,

Ilidaiwa kuwa Zitto Kabwe alizungumzia mauaji, yaliyotokea katika Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambayo yalisababishwa na vurugu kati ya Polisi na raia.

Serie A kurejea mwezi Juni
CAF kunusuru uchumi wa soka la Afrika