Mgombea wa uraisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Dokta John Pombe Magufuli amesema kuwa kama atashinda uchaguzi wa mwezi Oktoba atawashangaza watanzania .

Magufuli amesema hayo wilayani nzega,Tabora  kuwa yuko tayari kutumia muda wake na juhudi kufanya kazi kwaajili ya watanzania ,na hatojali wanaokosoa mfumo wake wa uongozi .

“Najua matatizo ya watanzania na ninataka kuwahakikishia yanatatuliwa japo wapinzani watasema ,nachotaka ni kuona wananchi wanapata  huduma za jamii,” alisema Magufuli

“matusi ninayoyapata ni majibu mazuri kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu , nitawashangza kama mtachagua CCM kuongoza miaka mingine mitano,” alisisitiza

Nzega ni moja ya maeneo yanayonufaika na mradi wa maji wenye thamani ya Bilioni 600 unaounganisha maji toka ziwa Victoria.

Leo Septemba 3 Rais Magufuli anaendelea kunandi sera zake mkoani shinyana .

Katwila ajivunia kikosi chake, ahimiza mapambano 2020/21
Simba SC, Young Africans patachimbika 2020/21

Comments

comments