Klabu ya Chelsea imekubali kulipa Pauni 1 milioni kama fidia ya kunasa makocha wengine kutoka Brentford ili wakapige kazi Stamford Bridge, imeelezwa.

Hilo limekuja licha ya kwamba Kocha Mauricio Pochettino alisema makocha hao hawana umuhimu wowote wa kuletwa kwenye timu.

Sasa kinachoelezwa ni Kocha Bernardo Cueva atawasili Stamford Bridge mwishoni mwa msimu akitokea Brentford, na The Blues imelipa Pauni 1 milioni kupata huduma yake.

Mmexico huyo, mwenye umri wa miaka 36, alijiunga Brentford akitokea Chivas, Septemba 2020 na awali alikuwa akifanya kazi ya kukusanya takwimu za kiufundi.

Ceva amekrwa na umuhimi mkubwa kweye timu hiyo chini ya kocha Thomas Prank na aliisaidia kupanda kutoka kwenye Championship hadi Ligi Kuu England.

Bilionea na mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly anataka kuboresha Benchi lao la ufundi hivyo, wameamua kumchukua kijana huyo akaongeze nguvu Stamford Bridge.

Anthony Barry ndiye aliyekuwa anafanya kazi ambayo atakwenda kufanya Cueva huko Chelsea, lakini kocha huyo aliachana na The Blues miezi 11 iliyopita na kwenda kuungana na Thomas Tuchel huko Bayern Munich.

Cueva atakwenda kuongeza idara ambayo itakuwa imeboreshwa zaidi na wakurugeni wa michezo Laurence Stewart na Paul Winstanley.

Kocha Pochettino ataletewa watu hao ili kuboresha Benchi lake la ufundi kwa msimu ujao.

Kamati yahimiza matumizi ya Gesi asilia Viwandani
Dkt. Biteko: Viongozi Serikalini tatueni kero za Wananchi