Shughuli za Bandari Nchini zimekuwa zikikua na kuongezeka, hali ambayo imechangia ongezeko la watumiaji wa usafiri na usafirishaji tofauti na miaka ya nyuma na hivyo kuwepo kwa abiria wengi wanaokadiriwa kufikia 5,000 hadi 8,000 kwa siku, ambapo idadi hiyo fufikia abiria hadi 10,000 kwa siku kwa kipindi cha sikukuu.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini, Plasduce Mbossa, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema kiuhalisia miundombinu iliyopo kwa eneo la Zanzibar haikidhi mahitaji ya sasa kutokana na ukweli kuwa ilijengwa miaka ya nyuma wakati kulikuwa na idadi ndogo ya wasafiri.

Amesema, “ni kweli lazima tukiri kwamba ile miundombinu iliyopo pale ikilinganishwa na idadi ya abiria wanaopita haliwezi tena kudhibiti hiyo hali na kwa wasiofahamu ni kwamba Wataali wanapita kwenda kule, Viongozi wetu wanapita pale na hilo limeonekana na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari na siyo tu ya Dar es Salaam na tulianza kufanya matengenezo.”

Hata hivyo, mesema si kweli kwamba mamlaka imeshindwa kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa abiria kiasi cha kutokea kwa malalamiko kwa wasafiri wanaotumia lango la kusafiria Zanzibar na Bara, kwani Boti zinazofanya safari na idadi ya wasafiri hufahamika hivyo haiwezekani mtu asiyesafiri akaingia eneo lile bila utaratibu.

Ancelotti: Real Madrid ina nafasi kubwa Ulaya
Rekodi zinaibeba Young Africans CAF