Mwenyekiti wa Bunge Marathon na Mbunge wa Makete Mkoani Njombe, Festo Sanga ameziomba taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za ujenzi wa Shule ya Bunge ya Wavulana kwa lengo la kukuza elimu.

Akuzungumza na Waandishi wa Habari hii leo Aprili 9, 2024 Bungeni Jijini Dodoma Sanga amesema wanawaomba Watanzania na Taasisi mbalimbali kujitokeza katika kufanikisha jambo hilo.

Amesema, “sisi bunge tunaziomba taasisi kutuunga mkono fedha au vifaa na tumeshaanza kupokea fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kutusapoti kuhakikisha shule inakamilika kama ambavyo tumepanga.”

Hata hivyo, amesema lengo la Marathon hiyo ni kukusanya shilingi Bilioni 3 ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo kwa lengo la kukamilisha maono ya Spika Dkt. Tulia Akson na kwamba tayari Shule ya Wasichana ilikwisha jengwa.

Mo Dewji, Benchikha kusajili Simba SC
Ukwepaji majukumu wachagiza wimbi la watoto wa mitaani