Mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa wa soka Tanzania Bara Young Africans, Mwinda Ramadhani amesema anafurahishwa na kiwango cha timu hiyo kwa sasa.

Mwinda ambaye kwa muda mrefu sasa anaishi Uingereza, amesema kuwa amekuwa akifuatilia baadhi ya mechi za timu yake hiyo ya zamani inapocheza na kusema kwa sasa wako kwenye kiwango bora.

Amesema Young Africans tangu msimu uliopita walipofika Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika wamekuwa kwenye mwendelezo mzuri wa kiwango chao.

“Nipo huku Uingereza nina muda mrefu sasa lakini kila nikipata nafasi naifuatilia Young Africans, hata mchezo dhidi ya Simba SC Jumamosi (Aprili 20) niliufuatilia.

“Wanacheza soka la kasi na kuonana na tangu msimu uliopita baada ya kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, nawaona wako kwenye mwendelezo mzuri wa kiwango chao,” amesema Mwinda aliyejiunga na Young Africans akitokea Pamba ya Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Mwinda aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 1987 na 1988 ameongeza kuwa anaiona timu hiyo ikifanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

TPLB: Ratiba Ligi Kuu haitavurugwa
Balozi Kusiluka: Uzoefu utumike kuharakisha mabadiliko