Mweka hazina wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, Sally Bolo ameomba msamaha kwa niaba ya beki wa Simba SC na Raia wa nchi hiyo, Joash Onyango Achieng ambaye alisababisha kufungwa mabao mawili katika ushindi wa Raja Casablanca 3-1 dhidi ya Simba SC nchini Morocco.
Simba SC ilicheza mchezo huo ugenini usiku wa kuamkia leo Jumamosi (April Mosi) mjini Casablanca, huku ikiwa na tiketi mkononi ya kucheza Robo Fainali kupitia Kundi C, linaoongozwa na Raja Casablanca yenye alama 16, ikifuatiwa na wababe hao wa Msimbazi wenye alama 09, Horoya AC ya Guinea imemaliza ikiwa na alama 07 na Vipers SC ya Uganda inaburuza mkia kwa kuwa na alama 02.
Sally amesema Onyango alikuwa mchezaji wa zamani wa Gor iliyokuwa inalelewa na Kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ambaye kwa sasa anaongoza maandamano yanayofanyika nchini humo kila siku za Jumatatu na Alhamisi hivyo imechangia Onyango kuwa na kiwango cha chini katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo Jumamosi (April Mosi).
“Tunaomba Wanasimba mkubali msamaha wetu kwa niaba ya Onyango, hakukusudia kusababisha bao la kwanza na la pili. Ni hali ya game,” ameandika Sally kwenye ukurasa wa Twitter
Simba SC inasubiri Droo ya Robo Fainali Jumatano (April 05) ili kufahamu mpinzani wa hayia hiyo ambayo itapigwa mwishoni mwa mwezi huu, kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.
Ni Dhahir Simba SC itavaana na mmojawapo wa vinara wa Kundi A, B au D.