Hofu kubwa inazidi kutanda kwa baadhi ya vigogo na viongozi wa umma juu ya mpango mpya ulioanzishwa na Serikali wa kuhakiki mali zao.
Aidha, hofu hiyo inatokana na uwekaji wa mfumo mpya Serikalini wa kufuatilia taarifa za kweli za mali za viongozi wa umma na kutunzwa vizuri kupitia mifumo ya kielektroniki.
Utekelezaji wa mpango huo wa uboreshaji wa taarifa za mali za viongozi wa umma, ndio unaowapa hofu viongozi na vigogo hao kwa sababu unawaweka katika wakati mgumu wale wenye tabia ya kuficha ukweli kuhusu mali wanazomiliki.
Hivi karibuni Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayojihusisha na utunzaji wa na ufuatiliaji juu ya taarifa zinazowasilishwa na na viongozi wa umma, imeunda mfumo wa kielektroniki wa menejimenti ya taarifa za kimaadili.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema kuwa mfumo huo mpya utarahisisha upatikanaji wa taarifa bora na kwa wakati.