Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Agostino Lyatonga Mrema amewaonya wanasiasa na baadhi ya watu ambao wamekuwa na tabia ya kumsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kusema kuwa kufanya hivyo ni kutenda kosa.
Ameyasema hayo mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam alipohudhuria ibaada ya shukrani katika kanisa la Siloam lililopo Mbezi beach, huku akijitolea mfano yeye mwenyewe kwa kunusurika kufungwa mara baada ya kumsema Rais wa awamu ya tatu mwaka 1996.
“Jamani naomba niwaonye hasa hawa wanao msema sema Rais kwa maneno mabaya, Rais wa nchi sio wa kuchezewa chezewa, anatakiwa aheshimiwe kwa kazi kubwa anayoifanya, kwani tumepata yule ambaye siku zote tulikuwa tukiomba usiku na mchana atusaidie,”amesema Mrema.
Hata hivyo, Mrema aliwaasa waumini wote kuongeza juhudi za kuwaombea viongozi mbalimbali wa Serikali kwani wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanaitumikia jamii.