Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeweka wazi kuwa mara baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya Raja Casablanca, safari hii hawataki utani watakapokutana na Vipers SC wakiwa nyumbani katika uwanja huo huku wakisema kuwa timu hiyo wataipelekea pumzi ya moto.

Simba SC katika mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0, mchezo wao wapili wakiwa nyumbani wanatarajiwa kucheza kesho Jumanne dhidi ya Vipers.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed amesema wamejifunza kutokana na makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo huo, na sasa wamejipanga kushinda katika Uwanja wa nyumbani dhidi ya Vipers SC.

“Mchezo wa kwanza ni kweli tulipoteza tukiwa nyumbani dhidi ya Raja Casbalanca tukafungwa mabao 3-0.”

“Safari hii niwaambie tu Vipers wamejichanganya kwani tutawapelekea pumzi ya moto na hakika lazima tupate matokeo mazuri ya kuwafurahisha Wanasimba wote ambao wamekata tamaa.”

“Bado tuna michezo miwili ya nyumbani, lazima tuitumie vizuri nafasi hii kwani naamini Simba kufika robo fainali ni kawaida kwake, hivyo Wanasimba tunawaomba mje kwa wingi kushangilia chama lenu ili tuwapige vizuri Vipers kwa Mkapa,” amesema Ahmed Ally

Mepema leo Jumatatu (Machi 06) Kikosi cha Vipers SC kiliwasili jijini Dar es salaam, tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC ambayo imekuwa kwenye maandalizi tangu Ijumaa (Machi 03), baada ya kumaliza mchezo wa 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya African Sports ya Tanga iliyokubali kufungwa 4-0, Uwanja wa Uhuru.

Yacouba Sogne awajibu kwa vitendo Ligi Kuu
Young Africans yapanga kuishangaza Afrika