Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amepanga kubadili kila kitu kuhusu mbinu na aina ya mfumo wa uchezaji ikiwa ni maalum kwa ajili ya mchezo wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Vipers SC ya Uganda.

Miamba hiyo ya Afrika Mashariki itapapatuana kesho Jumanne (Machi 07), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, baada ya kukutana mwishoni mwa juma lililopita nchini Uganda na Simba SC kuibuka na ushindi wa 1-0.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema kuwa analazimika kubadili mfumo kwa lengo la kupata ushindi wa mabao mengi nyumbani.

Amesema kuwa mfumo aliopanga kuutumia ni ule wa wa 4-3-3 badala 4-2-3-1 ambao ameona haumpi matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa mfumo huo mpya wa 4-3-3 uliokuwa unatumia na Kocha msaidizi Juma Mgunda atatumia washambuliaji wawili wenye viwango bora ili wapate matokeo mazuri.

“Hivi sasa natengeneza timu, hivyo ni lazima nitumie kila mfumo na ule utakaokuwa mzuri na kutupa ushindi, basi tutaendelea nao.”

“Kuelekea mchezo wetu dhidi ya Vipers SC, nitabadili mfumo kwa kuwatumia washambulia watatu kwa lengo la kupata ushindi wa mabao mengi.”

“Ninao washambuliaji wengi bora akiwemo John Bocco, Moses Phiri, Jean Baleke hivyo sina hofu” amesema Robertinho.

Mepema leo Jumatatu (Machi 06) Kikosi cha Vipers SC kiliwasili jijini Dar es salaam, tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC ambayo imekuwa kwenye maandalizi tangu Ijumaa (Machi 03), baada ya kumaliza mchezo wa 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya African Sports ya Tanga iliyokubali kufungwa 4-0, Uwanja wa Uhuru.

Young Africans yapanga kuishangaza Afrika
Tanzania Prisons yaivizia Namungo FC