Mlinda mlango wa Taifa Stars na klabu ya Azam FC, Aishi Manula amekiri kuwa hana namba ya kudumu katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania lakini hafanyi makosa anapopata nafasi.

Manula amesema amecheza mechi chache sana zikiwemo zile za Taifa Stars dhidi ya Chad, Harambee Stars ya Kenya na mechi ya juzi dhidi ya Nigeria.

” Kwanza ninashukuru kwa kupongezwa na nyota wa Nigeria kina Victor Moses, Ahmed Musa na Mikel Obi pamoja na wadau wengine lakini ni kawaida yangu kutofanya makosa ninapopewa nafasi.”

Manula alikuwa katika kiwango bora dhidi ya Nigeria kwa kuokoa michomo hatari ya washambuliaji wa Nigeria kiasi cha kutajwa mchezaji bora wa mchezo.

Video: Kamanda Sirro atoa taarifa ya ujambazi, Watatu wakamatwa na silaha 23, risasi 835
Sheria Ya Kuwalinda Watoa Taarifa Za Uhalifu Na Mashahidi Yaanza Kutumika