Kundi la kigaidi la Al Shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi lililofanyika Jumanne Usiku katika eneo la Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Kamishina wa Mandera aliiambia CNN kuwa washambuliaji waliwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 11 katika eneo hilo lililokaliwa na wafanyakazi katika mashimo ya mawe.

Nkoyo, alieleza kuwa mashambulizi yalianza majira ya saa saba usiku ambapo washambuliaji walitumia vilipuzi kufungua geti kubwa katika eneo hilo kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo. Alisema watu wengi walikuwa wamelala nje ya nyumba kukwepa joto lakini mashambulizi yalipoanza walioweza kukimbilia ndani walifanya hivyo. Hata hivyo, washambuliaji waliwafuata ndani na kuwaua baadhi yao.

Kumekuwa na taarifa kuwa serikali ya Kenya ilipata taarifa za kijasusi mapema kuwa kungeweza kutokea shambulizi la kigaidi katika eneo hilo na kwamba hawakuchukua hatua.
\
Taarifa hizo zimekanushwa vikali na serikali ya nchi hiyo na kueleza kuwa wangepata taarifa hizo mapema wasingepuuzia hata kidogo na kwamba wangefanya kila wawezalo kuzuia tukio hilo.

Kundi la kigaidi la Al Shabaab lilitangaza kuwa litafanya mashambulizi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, wakilenga Kenya, Uganda na Somalia.

Mayweather Avuliwa Ubingwa Wa Dunia
Diamond akosoa makundi yanayomshindanisha na Ali Kiba