Jeshi la Polisi Katavi linawashilikia watu wawili Dutu Maige (30) na Yusuph Sitta (32) kwa tuhuma za kumuua mama na mtoto wake mwenye umri wa miezi minne kisha miili yao kuifukia kwenye shimo katika pori la Kalilankulu lililopo wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamadi ameseme walipokea taarifa Machi 8 mwaka huu kutoka kwa Paschal Masheku mkazi wa kijiji cha Sante Maria kuwa binti yake huyo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu Julai 2021 akiwa amebeba mtoto wake.

Kamanda Hamad amesema baada ya taarifa hiyo walianza upelelezi wa kina ambapo Machi 9, 2022 walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao waliohusikana na tukio hilo ambapo moja kati ya watuhumiwa hao Yusuph Sitta ni mume wa marehemu.

Aidha chanzo cha tukio hilo ni kugombea mpunga ambao ni gunia 60 na walikuwa wakishtakiana mara kwa mara kwa watendaji wa kijiji ili kujua nani mmiliki halali wa mpunga huo.

Pia amesema awali miili ya marehemu hao ilikutwa kwenye pori ikiwa imeharibika kwa kushambuliwa na fisi na baadae ilifanyiwa uchunguzi na madaktari wa magereza kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kuzikwa.

Watuhumiwa hawakuishia hapo baada ya mazishi yaliyofanywa na jeshi la polisi,wao warirudi tena baadae na kufukua miili ya marehemu kisha kuichoma moto na kuipeleka sehemu nyingine ili kupoteza ushahidi.

Halmashauri zaaswa kusimamia miradi
Bahati nasibu na mifuko inainua michezo Tanzania