Hatimae meneja wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta Amatriain, amemjibu kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil, kufuatia waraka aliousambaza kwenye mitandao ya kijamii mapema juma hili.

Ozil alisambaza waraka wa kuachwa kwake katika mtandao wa kijamii baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa Arsenal imemuengua kwenye orodha ya wachezaji watakaiwakilisha klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu.

Arteta amesema Ozil ameshindwa kumuheshimu kwa tukio hilo, huku akimtaka ajilaumu mwenyewe kwani hajatimiza majukumu yake kama mchezaji.

Meneja huyo ambaye aliwahi kutumikia Arsenal kuanzia mwaka 2011 hadi 2016 amesema, Ozil ameleta vita ndani ya klabu ambayo haina ukweli, kwa kulituhumu benchi la ufundi kwa kukosa heshima na kuona thamani yake.

Arteta amesisitiza kuwa, Ozil hana mtu wa kumlaumu zaidi ya yeye mwenyewe, akimaanisha kuwa kiungo huyo kutoka amemalizana rasmi na klabu hiyo.

“Kitu kinachotokea kwa Ozil kwa sasa si kitu kipya. Hali niliyomkuta nayo wakati najiunga na klabu hii ilikuwa ngumu, mambo haya yamekuwa yakitokea kwa miaka minane sasa.”

“Kazi yangu ni kuimarisha viwango vya wachezaji kuleta timu bora uwanjani, lakini kwa sasa nahisi kama nimefeli. Nilimuhitaji Ozil mwenye kiwango bora na wakati tukimaliza mchakato, sikuwa na uwezo wa kumaliza hilo kwa ubora kwa sababu nilitakiwa kufanya uamuzi na kumwacha nje ya kikosi.”

“Hilo halihusiani na tabia ya mtu wala suala la mshahara kama ambavyo nimekuwa nikisoma katika mitandao. Hilo halina ukweli wowote.”

“Nimeajiriwa kama kocha kwa ajili ya kushinda mechi za klabu hii na natakiwa kufanya uamuzi kupata timu bora kutoka katika timu hii.” Amesema Arteta.

Arteta usiku wa kuamkia leo alikiongoza kikosi cha Arsenal kushinda mchezo waked wa kwanza wa UEFA Europa League kwa kuichabanga Rapid Wien mabao mawili kwa moja.

52 waitwa Ngorongoro Heroes
Wababe wa Israel wamsajili Novatus Dismas

Comments

comments