Mahakama ya Rufani Tanzania, imemhukumu kunyongwa mpaka kufa aliyewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Bageni, ikiwa ni hukumu ya kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha vifo vya wafanyabiashara watatu kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kesi hiyo imedumu kwa muda wa miaka kumi huku maafisa kadhaa wa jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wawili wakihusishwa kwenye kashfa hiyo ya mauaji, kabla ya hukumu kutolewa Septemba 16, 2016 na Mahakama ya Rufani Tanzania.

Wakili wa kujitegemea Gabriel Kambona kupitia kituo cha Azam TV ameizungumzia hukumu ya kunyongwa ambapo amesema kuwa imekuwepo tangu kipindi cha ukoloni na imerithiwa kutoka kwa Wajerumani ambao walikuwa wakiitekeleza. Bofya hapa kusikiliza #USIPITWE

Video: Prof. Benno Ndulu akitoa taarifa kamili ya hali ya uchumi Tanzania
Barnaba aeleza jinsi Mastaa walivyoukataa wimbo wa ‘Yule’ uliomtoa Ruby