Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amezungumzia sakata zima kuhusu Nchi za Afrika kubakia au kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC).

Waziri Mahiga amesema katika mkutano wa nchi za Afrika waliitaja mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyopo Arusha ipewe nafasi ya kusikiliza kesi ambazo zingepelekwa mahakama kuu ya ICC.

“Kulikuwa na mjadala mkali sana wengine wanasema Waafrika wote tujitoe mahakama ya ICC, lakini wengine wakasema tulipoingia kila mmoja aliingia mwenyewe kwahiyo hatuwezi kusema tujitoe wote kwa pamoja, anayetaka kutoka atoke mwenyewe kama aliyoingia mwenyewe na kuweka mkataba” – Waziri Mahiga

Vipimo Vyaonyesha Damu Kuganda Kwenye Jicho La Haji Manara
Joseph Omog Awakataa Wachezaji Wa Kigeni Simba SC