Mwimbaji wa kike wa Kenya, Avril ameweka wazi kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni mjamzito na mwenye furaha ya kutakakumkaribisha duniani mtoto wake.

Mkali huyo wa ‘Chokoza’ ambaye amekuwa akipost kwenye mitandao ya kijamii picha zinazoonesha maisha yake ya uchumba na mwanaume wa Afrika Kusini, amepost picha ya nguo na kiatu cha mtoto kwenye Instagram na kuandika “Cute”.

Baadhi ya watu maarufu na marafiki wa mwimbaji huyo wamejibu kwa kumpongeza kupitia mtandao huo. Swali la Nchakali lilimfanya Avril kufunguka zaidi na kueleza wazi kuwa anamleta mtoto atakayecheza na Zion (mtoto wa NchaKali).

“Only you would say that…. Zion’s playmate asap.” Avril alimjibu NchaKali.

P Diddy amchapa 50 Cent fimbo ya kiutu-uzima
Chadema Wakutana Kwa Dharura Kujadili Joto La Uchaguzi Mkuu