Mmiliki wa label ya Bad Boy, rapper mkongwe P Diddy amemfunza adabu kiongozi wa kundi la G-Unit, 50 Cent aliyemdhihaki hivi karibuni kuhusu performance ya kundi la Bad Boy kwenye tuzo za BET mwaka huu.

Baada ya tuzo za BET 2015, rapper 50 Cent alisema kuwa P Diddy na wasanii wa zamani wa kundi la Bad Boy waliopanda jukwaani kukumbuka miaka 20 ya kundi hilo,hawakufanya chochote zaidi ya utumbo tu.

Hata hivyo, katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, P Diddy ameonesha utu uzima katika siku ya kuzaliwa ya 50 Cent ambapo alipost picha kwenye Instraram akiwa na rapper huyo na kumtakiaheri ya siku ya kuzaliwa kuonesha kuwa uhasama hauna maana kwake katika enzi hizi.

P Diddy alienda mbali zaidi na kumuita 50 Cent kama mfalme, hali iliyotafsiriwa kama dhihaka ya kiutu uzima.
“May GOD BLESS YOU WITH Many more BELOVED..and I sent you a lifetime supply of the Superior ultra premium @CIROC @ciroc !!! elebrate responsibly!!!! But all jokes aside birthdays are sacred! Happy Birthday KING! Love always PUFF..” aliandika P Diddy.

Diamond akosoa makundi yanayomshindanisha na Ali Kiba
Avril Aweka Wazi Ujauzito Wake