Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Azam FC, akitokea APR ya kwao.

Migi yuko Tanzania tangu katikati ya wiki iliyopita baada ya kuwasili kwa mazungumzo na amecheza mechi zote mbili za kirafiki mwishoni mwa Tanga, Azam FC ikishinda 1-0 mara zote dhidi ya African Sports na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.

Pamoja na kusaini, Migi atajiunga na kikosi cha APR kinachowasili Dar es Salaam Jumatano kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati inayoanza Jumamosi mjini hapa.

Hayo ni makubaliano ya klabu zote mbili, kwamba Migi ataanza kuichezea Azam FC baada ya michuano ya Kagame akiwa na APR.

Azam na APR zipo makundi tofauti kwenye michuano hiyo na labda zinaweza kukutana kuanzia Robo Fainali. Kundi A kuna wenyeji, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan, Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi C kuna Azam FC wa Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.

Real Madrid, Espanyol Ngoma Ngumu
Yanga Wamalizana na KMKM, Wamchukua kihalali Mudathir Khamis