Dereva wa timu ya Mercedes, Lewis Hamilton jana aliibuka mshindi wa michuano ya mbio za magari michuiano ya Russian Grand Prix.

Michuano hiyo ambayo ilikumbwa na ajali nyingi, ilishuhudia Hamilton akionyesha ujasiri wa hali ya juu, dhidi ya wapuinznai wake huku wengi akiamini huenda mambo yalikua mazuri kwake kutokana na mapungufu yaliyojitokeza dhidi ya washiriki wengine.

Kufuatia ushindi huo mkubwa, Hamilton anakaribia kutangazwa kuwa mshindi wa mwaka huu wa mbio za magari, na kama itakua hivyo, basi atafikisha ubingwa wa tatu wa dunia

Katika michuano ya jana, Hamilton alikuwa katika nafasi ya pili kuelekea dakika za mwisho za mashindano hayo kabla ya dereva mwenzake wa timu ya Mercedes, Nico Rosberg kukabiliwa na matatizo ya injini.

Kufuatia tatizo hilo Rosberg ambaye ni raia wa nchini Ujerumani alilazimika kujiondoa kwenye mshike mshike huo kutokana na kushindwa kupata kasi ya kukimbiza gari lake.

Kwa upande wa dereva wa timu ya Ferrari, Sebastian Vettel alimpiku Rosberg kutoka katika nafasi ya pili katika jedwali la msimamo wa dereva bora msimu huu.

Dereva wa timu ya Force India, Sergio Perez alimaliza katika nafasi ya tatu baada ya dereva shupavu wa timu ya Ferrari, Kimi Raikkonen, kuhusika katika ajali mbaya na gari la Williams lililokuwa likiendeshwa na Valtteri Bottas katika mzunguko wa mwisho.

Hamilton ameshinda mashindano 9 msimu huu na hivyo anahitaji alama 9 pekee kutangazwa kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu.

Mashindano yajayo yamepangw akufanyika nchini Marekani, na kama Hamilton atarejea kufanya vyema na kufikia laama 9 anazokusudiwa basi atatimiza lengo la kuwa bingwa kwa mwaka 2015.

Angalia Video Mpya ya Vanessa Mdee – Never Ever
Shomari Kapombe Yu Mashakani