Baada ya kurejea katika kikosi cha AC Milan, Kevin Prince Boateng amekiri kuwa, aliota ndoto ya kwamba siku moja atarudi tena katika viunga vya Sansiro.

Kisha akabainisha kuwa, hatua yake hiyo imempa faraja ya kudumu kwa kile alichodai kuwa klabu hiyo ni sawa na mtoto aliyerejea nyumbani ambako kuna mikono salama ya wazazi.

“Hapa Sansiro ni kama nyumbani, kuna siku niliwaza juu ya kurudi tena hapa na asa ndoto yangu imetimia.”

“Uamuzi wangu huu nauchukulia kama ni wa kutimiza ndoto yangu ya siku nyingi na kwamba katika soka la zama hizi kucheza AC Milan ni sawasawa na kucheza katika klabu yoyote kubwa ulimwenguni,” amesisitiza Boateng.

Kiungo huyo mkonge alijiunga tena na AC Milan akitokea katika timu ya Schalke, ambapo klabu yake ya sasa ya AC Milan tayari imeshampa mkataba unaomfanya akipige katika dimba la Sansiro. Mkataba wake wa sasa ni miezi sita.

Boateng ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu za Totenham na Portsmouth, alijiunga na Schalke mwezi Agosti, mwaka 2013 lakini amekuwa akikabiliwa na tatizo la utovu wa nidhamu na kuingia katika mzozo na klabu yake ya sasa.

Schalke ilitangaza kuachana na kiungo huyo mwishoni mwa mwezi Desemba, hivyo kumsafishia njia ya kutua Rossoneri kwa mkataba mfupi wa miezi sita kwa ajili ya serie A.

AC Milan walikubali kumsainisha mkataba wa miezi sita kiungo Kevin Prince Boateng na mkataba wake unatarajiwa kufikia ukingoni mwezi Juni, mwaka 2016.

Cesc Fabregas Amfukuzisha Kazi Mfanyakazi Wa Chelsea
Marouane Fellaini Kuendelea Kusota Old Trafford