Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) imetoka  ambapo itaanza kutimua vumbi tarehe 19 Septemba, 2015 kwa timu 24 zinazoshiriki ligi hiyo kutoka katika mikoa mbali mbali nchini.

Ligi hiyo ya Daraja la kwanza inatarajiwa kumalizika Machi 12, 2016 ina makundi matatu yenye timu nane kwa kila kundi, kila kundi litacheza michezo saba nyumbani na ugenini na mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja kwenye Ligi Kuu ya Vodacom nchini.

Kundi A lina timu za African Lyon (Dar es salaam), Ashanti United (Dar es slaam), Friends Rangers (Dar es salaam), Kiluvya FC (Pwani), Polisi Dar (Dar es salaam), KMC FC (Dar es salaam), Mji Mkuu (Dodoma) na Polisi Dodoma (Dodoma).

Kundi B lina timu za Kurugenzi (Iringa), Burkinafaso (Morogoro), JKT Mlale (Ruvuma), Lipuli FC (Iringa), Ruvu Shooting (Pwani), Njombe Mji (Njombe), Kimondo  FC (Mbeya) na Polisi Moro (Morogoro).

Kundi C linaunda na timu za Panone FC (Kilimanjaro), JKT Oljoro (Arusha), Polisi Mara (Mara), Rhino Rangers (Tabora), Mbao FC (Mwanza), Polisi Tabora (Tabora), Geita Gold (Geita) na JKT Kanembwa (Kigoma).

TFF Yatuma Salamu Za Pongezi Kwa Bayi
Man City Wakubali Kutoa Mzigo