Mkutano wa Tatu wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili na kupitisha bajeti za Wizara mbalimbali pamoja na bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mkutano huo unaanza katika kipindi hiki ambacho Taifa lipo kwenye siku 21 za maombolezo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Bunge hilo pia litapitisha azimio la Bunge la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa Sita ya Tanzania.

Hata hivyo, Bajeti ya mwaka huu ni ongezeko la asilimia nne kutoka mwaka jana ambapo bajeti yake ilikuwa trilioni 34.88.

Ongezeko hilo la asilimia nne linatokana na mahitaji ya mfuko mkuu wa serikali ikijumuisha malipo ya deni la serikali.

Kwa mujibu wa muongozo wa bajeti uliotolewa na Serikali Februari mwaka huu na kusomwa Bungeni na Waziri wa Sheria na Katiba, Mwigulu Nchemba, ongezeko hilo limetokana na mahitaji ya upandishwaji wa madaraja na watumishi na ajira mpya.

Dkt. Tulia: Hizi kelele zinatoka wapi kwa jambo hili zito?
LHRC yalaani mauaji ya mtangazaji wa ITV