Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetumia sayansi na teknolojia mpya ya kurusha matangazo ambapo sasa matangazo yake yatapatikana kwa njia ya satellite yanayoviwezesha vituo vya redio na runinga nchini kupata matangazo yake bila kufunga mitambo yao katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge, vituo vya runinga nchini vitakuwa vinapata matangazo yake kupitia Sattelite Intelsat 17, nyuzi 66 upande wa Mashariki.

Hata hivyo, taarifa hiyo imefafanua kuwa hatua hiyo haiwazuii waandishi wa habari kuingia bungeni kwa ajili ya kuchukua habari na kuripoti.

Hii ndio namna ya kuyapata matangazo hayo ya Bunge kwa njia ya satellite:

SATELLITE: Intelsat 17 @ 66 East

FREQUENCY: 11024.2500MHZ

SYMBOLRATE: 3071.8 Mbps

POLARIZATION: Horizontal

FEC: 1/2

MODULATION: 4PHASE-QPSK

AUDIO: CH. 1…noneI, CH.2…none, CH.3…TV Audio na CH. 4…Radio

Kasi ya Magufuli kuwayoosha wenye nyumba za kupangisha
Takukuru kumrudisha kizimbani Mhando wa Tanesco