Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya amesema Watanzania wanaona fahari ya Bwawa la Mwalimu Nyerere, na kudai kuwa anatamani uendeshaji na ukamilikaji wa mradi huo uendane na thamani ya pesa iliyowekezwa.

Bulaya ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati ya mwaka wa fedha 2023/2023, ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Januari Makamba.

Amesema, “Watanzania wote wana fahari ya Bwawa la Mwalimu Nyerere, kwa sababu ni fahari ya nchi na matamanio ya wengi ni kuona uendeshaji na ukamilikaji wake unaendana na thamani iliyowekezwa.

Kukamilika kwa Bwawa hilo kutawezesha upatikanaji wa umeme kuwa wa uhakika, ambapo tayari Waziri Makamba amesema kila kijiji nchini kitakuwa na umeme ifikapo Juni 2024.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 2, 2023
Wataalamu Wizara ya Fedha, IMF kujadili athari za kiuchumi