Saa 48 baada ya Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS) kutengua maamuzi ya shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) kuifungia Manchester City kushiriki michuano ya bara hilo kwa miaka miwili, meneja wa klabu hiyo ya Etihad Pep Guardiola, ameibuka na kutoa kauli nzito.

Uongozi wa Manchester City ulikata rufaa CAS kupinga maamuzi ya UEFA, kwa kuamini hawakutendewa haki wakati wa kutangazwa hukumu mapema mwaka huu, kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na ulaghai mkubwa katika makusanyo ya mapato ya klabu (FFP), pamoja na kutotoa ushirikiano kwa timu iliyokuwa inafanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha mwaka 2012-2016.

Guardiola ameibuka na kusema shirikisho hilo la Soka Barani Ulaya linatakiwa kuiomba radhi klabu hiyo ya mjini Manchester, England kufuatia maamuzi ambayo ni dhahir yameonekana hayakua ya haki.

“Kilichofanyika ni haki, lakini makocha wote hapa ni lazima wajue kuwa tunahitaji haki na bila shaka haki imetendeka. Nadhani kuna haja ya sisi kuombwa radhi kwa makosa yao,” amesema Guardiola

“Nina furaha juu ya maamuzi hayo, nadhani ingetengeneza picha mbaya kwa klabu yetu lakini pia watu wamekuwa wakizungumza vibaya juu yetu kwa sababu ya ubora wetu uwanjani.”

Mwezi wa pili mwaka huu Uefa walitoa hukumu juu ya City ya kutoshiriki Michuano ya Ulaya hata kama wangefuzu lakini kufutwa kwa makosa kuna maanisha kuwa mwakani matajiri hao wa Jiji la Manchester watakuwa sehemu ya washindani kwenye michuano ya UEFA.

Waziri Mkuu arudi Ruangwa, Lukuvi Isimani
Kishindo cha Mdee, Matiko, Bulaya kura za maoni Ubunge