Hivi karibuni kulikuwa na taarifa zilizobaini kuwepo kwa harufu ya mpasuko mkubwa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutokana na uteuzi wa wabunge wa viti maalum uliomuacha nje mtoto wa kigogo wa chama hicho.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la kila siku nchini zilieleza kuwa Chadema ilivurugana kimyakimya kutokana na kusahaulika kwa jina la Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa Mzee Philemon Ndesamburo aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini na mwenye heshima kubwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.

Lucy ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge wa Bunge la kumi, alidaiwa kuwa alishinda katika kura za maoni za chama hicho lakini Kamati Kuu ilipangua jina lake na baadae kusaulika kwenye orodha ya wabunge wa viti maalum. Hali hiyo ilidaiwa kuzua taharuki kuwa huenda uongozi wa chama hicho haumtaki bungeni.

Hata hivyo, huenda mtafuruku huo ukawa umezimwa moja kwa moja jana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kumtaja Lucy Owenya kuwa mmoja kati ya wabunge wa viti maalum wa chama hicho, katika orodha ya majina matatu ya wabung wa viti maalum waliokuwa wamesalia kukamilisha idadi ya wabunge 113.

NEC ilitaja orodha ya ‘second selection’ ya viti maalum baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa majimbo yote yaliyokuwa yanasubiriwa, ambayo hajakufanya uchaguzi Oktoba 25.

Idadi ya wabunge wa viti maalum inapaswa kuwa asilimia 40 ya idadi ya wabunge waliochaguliwa kwa kura majimboni.

Inasikitisha: Kilichomtokea Mwanamke Aliyechapwa viboko hadharani kwa uzinzi
Exclusive: Jaffarai aeleza Magufuli alivyomvuta kuingia kwenye siasa, Ushauri wa Kufanikiwa Kibiashara na muziki wake (Audio)