Nyota wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani Chris Brown ameachia albam yake mpya inayoitwa ‘Heartbreak On A Full Moon’ yenye jumla ya nyimbo 45.

Albam hiyo ni ya nane kutoka kwa Chris Brown na ndani ya albamu hiyo amewashirikisha wasanii tofauti wakiwemo Future, Young Thug, Lil Yachty, Usher, Gucci Mane, R. Kelly, Verse Simmonds, Jhene Aiko, Kodak Black, Ty Dolla $ign, Dej Loaf na wengine wengi.

Ni mwaka mmoja na nusu sasa tangu mwezi Mei mwaka jana Chris Brown alipotoa wimbo wa Grass Ain’t Greener na kutangaza ujio wa albam mpya na sasa albam hiyo imetoka rasmi jana tarehe 31 mtandoni huku mashabiki wanaotaka kununua madukani wakitarajia kuipata albamu hiyo tarehe 3 mwezi Novemba.

Sikiliza nyimbo za albam hiyo hapa chini;

Rais Karia awapa pole Silabu FC
TFF kuzilipa timu ASFC mapema