Bondia Cosmas Cheka usiku wa jana(Dis 19) amelambishwa sakafu na bondia Vyanceslav Guchev wa Urusi katika pambano la raundi 12 la kuwania ubingwa wa IBF International lililofanyika mjini Moscow.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Chama Cha Ngumi za kulipwa Tanzania PST, Cosmas Cheka ameshindwa kwa pointi.

Pambano hilo la uzito wa kilogramu 59 lilishuhudiwa na maafisa kadhaa akiwemo balozi wa Tanzania nchini Urusi Mathew Kisamba.

Taarifa zinasema kwamba Cheka alicheza vizuri pambano hilo.

Eva Carneiro Hajakata Tamaa Dhidi Ya Chelsea
Mfahamu Mkali Wa Mabao Ligi Ya England, Jamie Vardy